Friday, February 26, 2016

Jifunze upishi wa katles




 



 MAHITAJI
A. Nyama ya kusaga                           Kilo 1
B. Viazi mbatata                                
C. Giligilani
D. Vitunguu maji na swaumu, tangawizi, hoho, keroti
E. Chumvi kiasi, ndimu
F. Binzari nyembamba, pilipili manga
G. Mayai                                                         4
H. Unga wa sembe/ngano
I. Mafuta ya kupikia uyapendayo

MAANDALIZI
Hatua Ya Kwanza
Chukua nyama yako ya kusaga weka katika sufuria, weka chumvi kiasi, tia ndimu, kitunguu swaumu, tangawizi na iache ichemke. Usiweke maji hata kidogo itaiva yenyewe na yale maji maji yake na uhakikiche yale maji yamekauka kabisa. Ipua na uweke pembeni ukisubiri ipoe.

Hatua Ya Pili
Menya viazi vyako mbatata na usafishe vizuri, baada ya hapo vikate kate na uviweke kwenye sufuria yako, Tia chumvi kiasi, tangawizi kiasi, virushe rushe na uweke jikoni tia na maji kiasi, funika na acha vichemke kwa muda (ila mimi napendelea kuweka na maji kiasi ili yakaukie kabisa hua sipendi baada ya viazi kuwiva nichuje maji). Vikisha iva na hakikisha havina maji anza kuvisaga, utaendelea kusanga mpaka upate ulaini unaoutaka wewe.

Hatua Ya Tatu
Katakata hoho, vitunguu maji, keroti katika mfumo ule ule wa vipande vidogo vidogo na ukimaliza hapo chukua mchanganyiko wako wa nyama na viazi uweke katika chombo kimoja, halafu chukua vitunguu maji, hoho, keroti ulivyo katakata tia kwenye mchanganyiko wako wa nyama na viazi, tia swau yako, kamulia tena ndimu, weka na unga wa binzari nyembamba na pilipili manga, katia na giligilani zako, sasa anza kuchanganya vyote kwa pamoja. Changanya chananya mpaka utakapo ona vyote vimechanganyika vizuri. Please test mchanganyiko wako kuoma kama mambo yapo poa.

Hatua Ya Nne
Andaa sahani zako za kuwekea madonde yako ya katres zinyunyuzie unga wa sembe ama ngano itategemea wewe wataka unga gani. Waweza tumia unga wa sembe au ngano. Ukisha maliza hapo chukua mchanganyiko wako na utengeneze style uipendayo kama vidualisho, CD-style finger style yote kheri tu. Baada ya hapo utaviviringisha katika unga wako uliouchagua wewe na utapanga kwenye sahani, utarudia hivyo katika vidude vyote. Next chukua mayai yako yale manne yavunje na kutia katika chombo safi at the same time unakua ushabandika kichomeo chako jikoni na ushaweka mafuta yako. Tumia moto wa wastani . Mafuta yakishapata moto kiasi cha wewe kuridhika chukua katres zako tia katika mayai zungusha zungusha ili mayai yaingie pande zote halafu tia kwenye kikaangio chako jikoni, rudia kafanya hivyo kwa katres zote zilizo baki na ukimaliza hapo mambo yatakua poa na tayari kujisevia.

Saturday, February 13, 2016

The Nyama Choma Festival Dar es Salaam 6th Dec

Vyakula 10 kwa kuimarisha ngozi yako

Wote tunapenda kuonekana warembo na vijana. Lakini inawezekana ukawa unajiharibu zaidi katika kujifanya uwe mrembo leo na kujiletea madhara makubwa yasiyotibika kesho. Pia, inawezekana unatumia hela nyingi na muda mwingi katika kuhakikisha ngozi yako inakuwa nyororo, nzuri, na ya kuvutia. Je, unafahamu kuwa kuna aina za vyakula vinavyosaidia katika kutunza ngozi yako?
Kama ambavyo unajitahidi kufuata kanuni za afya ili kuufanya mwili wako uwe vizuri – chakula bora, mazoezi mara kwa mara, kupumzika kwa muda mrefu – vivyo hivyo ngozi yako inatakiwa kutunzwa kutokana na kanuni asilia. Hapa tunakuletea vyakula vinavyotunza ngozi yako bila gharama yeyote.

1. Asali

honeyjar
Asali ni afya kwa binadamu, hutengenezwa na nyuki kwa viambato asilia. Chochote kile ambacho ni kizuri kwa afya yako ni nzuri kwa ngozi pia. Ngozi yenye afya inatakiwa kuhifadhi unyevunyevu ili kuzuia kukauka na kupasuka. Hii ndio sababu kubwa ya kutumia mafuta ili kuweka ngozi iwe na unyevunyevu. Asali husaidia kuleta na kuhifadhi unyevunyevu kwenye ngozi.
Ili kuweza kulinda ngozi, paka asali wakati wa kuoga, acha kwa muda kisha ioshe. Ni zoezi la muda mfupi linalohakikisha ngozi yako inanawiri vizuri.
Asali ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambavyo huzuia vijidudu (Bacteria) wanaozaliana kwenye ngozi.

2. Vyakula vya baharini

what-are-shellfish-foods
Kwa ujumla vyakula vya baharini ni vizuri kwa afya yako, lakini faida haishii kwenye afya ya mwili tu, bali inasaidia hata kwenye ngozi yako. Vyakula vingi vya baharini vina kiwango kikubwa cha Zinc na Omega-3 ambazo ni muhimu kwa afya ya ngozi yako.

Faida za Omega3

  • Kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi.
  • Kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi.
  • Husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi -  mzunguko mzuri wa damu mwilini ni muhimu kwa ngozi yenye afya.

Faida za Zinc kwa ngozi

  • Inasaidia kuondoa chunusi na harara kwa kuyeyusha homoni ya testosterone.
  • Inasaidia kuzalishwa kwa seli au chembe hai za mwili na kuondoa chembe zilizokufa. Hii inaifanya ngozi kung’aa na kuwa na mvuto.

 3. Mayai

Image result for mayai

 Nadhani si ajabu kusema kuwa yai ni kirutubisho muhimu kwa afya yako. Lakini afya yako huonekana kutokana na ubora wa ngozi yako. Yai lina virutubisho muhimu sana – iwe kiingi au ute – kwa afya ya ngozi yako. Kiini cha yai kina vitamin A, na B. Ute wa yai una protini nyingi ambayo ni muhimu pia kwa ngozi yako.
  • Tretinoin inayopatikana kwenye Vitamin A kwa ngozi yako ni kuwa inasaidia kuondoa chunusi na mikunjo ya ngozi.
  • Biotin inayopatikana kwenye Vitamin B ni muhimu kwa afya ya ngozi na kucha.
  • Protini inayopatikana kwenye ute wa yai ni muhimu kufanya ngozi kuwa nyororo na yenye kung’aa na kusaidia ngozi kujilinda vizuri na mionzi ya jua.

4. Matunda

citrus-fruits
Matunda yenye vitamin C – chungwa, limao na mengine mengi – ni muhimu kwa afya ya ngozi yako sababu inasaida kutengeneza collagen, aina ya protini inayotengeneza ngozi.
Vitamin C inasaidia kuondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi hivyo kuilinda ngozi yako kuzeeka mapema.

5. Shayiri

20120212_pbandbananaoatmeal4
Shayiri ina virutubisho muhimu vya kuisaidia ngozi yako. Hivi ni kama
  • Mafuta yanayolainisha ngozi
  • Polysaccharides ambayo huzuia kupasuka kwa ngozi kutokana na ukavu
  • Saponins, inayosaidia kusafisha ngozi na kuzuia fungus na vijidudu
  • Polyphenols inayozuia uvimbe wa ngozi
  • Protini inayojenga na kurutubisha ngozi
  • Wanga unaohifadhi unyevunyevu kwenye ngozi

6. Mboga za majani

arthritis2
Mboga za majani zina vitamini A nyingi sana. Vitamin A ni muhimu kwenye ngozi sababu ndio kitu kikubwa kwenye kusaidia ngozi kuzalisha seli mpya na kuondoa zile zilizokufa, hivyo kupunguza ukavu na kutunza ngozi na kuifanya kungara na kuvutia.

7. Shea Butter

sheabutter-thumbnail
Mafuta ya shea ni kirutubisho muhimu kinachotumika kwa muda mrefu sana katika kutibu magonjwa mengi, hasa katika nchi za Afrika. Mafuta ya shea yana triglycerides, mfano palmitic, stearic, oleic and linoleic fatty acids. Hivi ni muhimu katika kuleta unyevunyevu na kulinda ngozi kwa muda mrefu.

8. Karanga

nuts
Vyakula jamii ya karanga vina vitamin E ambayo ni muhimu katika kuzuia kuzeeka kwa ngozi hasa  kutokana na kupigwa sana na jua. Vitamin E pia husaidia ngozi kuhifadhi unyevunyevu na hivyo kuifanya ngozi kuwa inang’aa na nyororo.

9. Maziwa ya Mbuzi

326044212_640
Maziwa ya mbuzi yana Vitamin A, E na Lactic acid. Lactic acid husaidia kuondoa seli zilizokufa kwenye ngozi na kuacha ngozi ikiwa na seli zilizo hai, hivyo kuifanya iwe na afya.
Maziwa ya mbuzi pia yana  Caprylic Acid ambayo ni muhimu kwenye kupunguza kiwango cha asid kwenye ngozi – hii inasaidia kuzuia mazalia ya bakteria na vijidudu kwenye ngozi vilevile kusaidia ngozi kufyonza virutubishi kirahisi.

10. Nafaka isiyokobolewa

whole-grains
Vyakula visivyokobolewa vina virutubisho vingi zaidi na vina faida kubwa zaidi kwenye afya ya mwili pamoja na ngozi yako. Mfano ngano ni chanzo muhimu cha Vitamin B – Biotin ambayo inasaidia seli kutengeza mafuta na hivyo kuzuia kupasuka na kukatika kirahisi.

Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu





 juices.jpg
Katika ulimwengu wa vyakula, inafahamika na kuaminika kuwa chakula ni dawa. Chakula unachokula leo ndicho kinachoamua hali yako ya kiafya kesho. Unaweza kuishi bila kuugua kama ukila vyakula vyote muhimu vinavyohitajika mwilini.

Leo nitakutajia orodha ya juisi zilizotengenezwa kwa matunda na mboga na fadia zake mwilini. Katika orodha hii, utaona kuna mchanganyiko wa matunda au mboga mbili hadi nne na kazi zake mwilini, zikitumika kama tiba au kinga ya magonjwa.

KAROTI, TANGAWIZI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda hayo matatu huondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Tufaha ndiyo apple kwa Kiingereza.

TUFAHA, TANGO NA FIGILI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya ni kinga dhidi ya saratani, huondoa lehemu (cholestrol) mwilini, husafisha tumbo na pia huondoa maumivu ya kichwa.

NYANYA, KAROTI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya ngozi ya mwili mzima kuwa nyororo na huondoa harufu mbaya mdomoni.
TANGO CHUNGU,

TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili.

CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana.

NANASI, TUFAHA NA TIKITIMAJI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo.

TUFAHA, TANGO NA ‘KIWI’
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni aina ya matunda ambayo hujulikana pia kama ‘matunda-damu’.

PEASI NA NDIZI

Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Inawafaa sana wagonjwa wa kisukari na inaweza kuwa sawa na kinga dhidi ya ugonjwa huo.

KAROTI, PEASI, TUFAHA NA EMBE
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huzuia athari ya sumu mwilini, hupunguza shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.

MASEGA YA ASALI, ZABIBU, TIKITIMAJI NA MAZIWA
Juisi yenye mchanganyiko huu huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C na Vitamin B2 ambazo huimarisha chembechembe hai na kinga ya mwili.

PAPAI, NANASI NA MAZIWA
Juisi hii ina kiwango kikubwa cha Vitamin C, E na madini chuma. Huimarisha rangi ya ngozi na mfumo wa usagaji wa chakula tumboni.

NDIZI, NANASI NA MAZIWA

Juisi hii yenye kiasi kikubwa cha vitamini na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huzuia tatizo la ukosefu wa choo.

Ili kupata faida hizo zilizoainishwa katika kundi la matunda hayo, usafi wa matunda yenyewe hauna budi kuzingatiwa wakati wa kutayarisha juisi yake. Vilevile hakikisha unatumia matunda yaliyoiva vizuri.

Unaweza kutumia mashine maalumu ya kukamulia matunda (blender) au kutumia njia ya asili ya kutwanga kwa kinu maalumu na kupata juisi hiyo. Kama utaongeza sukari, inashauriwa kuweka kiasi kidogo sana. Ni bora zaidi usipoweka sukari, kwa sababu matunda mengi yana sukari ya asili.