MAHITAJI
A. Nyama ya kusaga
Kilo 1
B. Viazi mbatata
C. Giligilani
D. Vitunguu maji na swaumu, tangawizi,
hoho, keroti
E. Chumvi kiasi, ndimu
F. Binzari nyembamba,
pilipili manga
G. Mayai
4
H. Unga wa sembe/ngano
I. Mafuta ya kupikia
uyapendayo
MAANDALIZI
Hatua Ya Kwanza
Chukua nyama yako ya
kusaga weka katika sufuria, weka chumvi kiasi, tia ndimu, kitunguu swaumu,
tangawizi na iache ichemke. Usiweke maji hata kidogo itaiva yenyewe na yale
maji maji yake na uhakikiche yale maji yamekauka kabisa. Ipua na uweke pembeni
ukisubiri ipoe.
Hatua Ya Pili
Menya viazi vyako
mbatata na usafishe vizuri, baada ya hapo vikate kate na uviweke kwenye sufuria
yako, Tia chumvi kiasi, tangawizi kiasi, virushe rushe na uweke jikoni tia na
maji kiasi, funika na acha vichemke kwa muda (ila mimi napendelea kuweka na
maji kiasi ili yakaukie kabisa hua sipendi baada ya viazi kuwiva nichuje maji).
Vikisha iva na hakikisha havina maji anza kuvisaga, utaendelea kusanga mpaka
upate ulaini unaoutaka wewe.
Hatua Ya Tatu
Katakata hoho,
vitunguu maji, keroti katika mfumo ule ule wa vipande vidogo vidogo na
ukimaliza hapo chukua mchanganyiko wako wa nyama na viazi uweke katika chombo
kimoja, halafu chukua vitunguu maji, hoho, keroti ulivyo katakata tia kwenye
mchanganyiko wako wa nyama na viazi, tia swau yako, kamulia tena ndimu, weka na
unga wa binzari nyembamba na pilipili manga, katia na giligilani zako, sasa
anza kuchanganya vyote kwa pamoja. Changanya chananya mpaka utakapo ona vyote
vimechanganyika vizuri. Please test mchanganyiko wako kuoma kama mambo yapo
poa.
Hatua Ya Nne
Andaa sahani zako za
kuwekea madonde yako ya katres zinyunyuzie unga wa sembe ama ngano itategemea
wewe wataka unga gani. Waweza tumia unga wa sembe au ngano. Ukisha maliza
hapo chukua mchanganyiko wako na utengeneze style uipendayo kama vidualisho,
CD-style finger style yote kheri tu. Baada ya hapo utaviviringisha katika unga
wako uliouchagua wewe na utapanga kwenye sahani, utarudia hivyo katika vidude
vyote. Next chukua mayai yako yale manne yavunje na kutia katika chombo safi at
the same time unakua ushabandika kichomeo chako jikoni na ushaweka mafuta yako.
Tumia moto wa wastani . Mafuta yakishapata moto kiasi cha wewe kuridhika chukua
katres zako tia katika mayai zungusha zungusha ili mayai yaingie pande zote
halafu tia kwenye kikaangio chako jikoni, rudia kafanya hivyo kwa katres zote
zilizo baki na ukimaliza hapo mambo yatakua poa na tayari kujisevia.
No comments:
Post a Comment