Kama ambavyo unajitahidi kufuata kanuni za afya ili kuufanya mwili wako uwe vizuri – chakula bora, mazoezi mara kwa mara, kupumzika kwa muda mrefu – vivyo hivyo ngozi yako inatakiwa kutunzwa kutokana na kanuni asilia. Hapa tunakuletea vyakula vinavyotunza ngozi yako bila gharama yeyote.
1. Asali
Asali ni afya kwa binadamu, hutengenezwa na nyuki kwa viambato asilia. Chochote kile ambacho ni kizuri kwa afya yako ni nzuri kwa ngozi pia. Ngozi yenye afya inatakiwa kuhifadhi unyevunyevu ili kuzuia kukauka na kupasuka. Hii ndio sababu kubwa ya kutumia mafuta ili kuweka ngozi iwe na unyevunyevu. Asali husaidia kuleta na kuhifadhi unyevunyevu kwenye ngozi.
Ili kuweza kulinda ngozi, paka asali wakati wa kuoga, acha kwa muda kisha ioshe. Ni zoezi la muda mfupi linalohakikisha ngozi yako inanawiri vizuri.
Asali ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambavyo huzuia vijidudu (Bacteria) wanaozaliana kwenye ngozi.
2. Vyakula vya baharini
Kwa ujumla vyakula vya baharini ni vizuri kwa afya yako, lakini faida haishii kwenye afya ya mwili tu, bali inasaidia hata kwenye ngozi yako. Vyakula vingi vya baharini vina kiwango kikubwa cha Zinc na Omega-3 ambazo ni muhimu kwa afya ya ngozi yako.
Faida za Omega3
- Kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi.
- Kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi.
- Husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi - mzunguko mzuri wa damu mwilini ni muhimu kwa ngozi yenye afya.
Faida za Zinc kwa ngozi
- Inasaidia kuondoa chunusi na harara kwa kuyeyusha homoni ya testosterone.
- Inasaidia kuzalishwa kwa seli au chembe hai za mwili na kuondoa chembe zilizokufa. Hii inaifanya ngozi kung’aa na kuwa na mvuto.
3. Mayai
- Tretinoin inayopatikana kwenye Vitamin A kwa ngozi yako ni kuwa inasaidia kuondoa chunusi na mikunjo ya ngozi.
- Biotin inayopatikana kwenye Vitamin B ni muhimu kwa afya ya ngozi na kucha.
- Protini inayopatikana kwenye ute wa yai ni muhimu kufanya ngozi kuwa nyororo na yenye kung’aa na kusaidia ngozi kujilinda vizuri na mionzi ya jua.
4. Matunda
Matunda yenye vitamin C – chungwa, limao na mengine mengi – ni muhimu kwa afya ya ngozi yako sababu inasaida kutengeneza collagen, aina ya protini inayotengeneza ngozi.
Vitamin C inasaidia kuondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi hivyo kuilinda ngozi yako kuzeeka mapema.
5. Shayiri
Shayiri ina virutubisho muhimu vya kuisaidia ngozi yako. Hivi ni kama
- Mafuta yanayolainisha ngozi
- Polysaccharides ambayo huzuia kupasuka kwa ngozi kutokana na ukavu
- Saponins, inayosaidia kusafisha ngozi na kuzuia fungus na vijidudu
- Polyphenols inayozuia uvimbe wa ngozi
- Protini inayojenga na kurutubisha ngozi
- Wanga unaohifadhi unyevunyevu kwenye ngozi
6. Mboga za majani
Mboga za majani zina vitamini A nyingi sana. Vitamin A ni muhimu kwenye ngozi sababu ndio kitu kikubwa kwenye kusaidia ngozi kuzalisha seli mpya na kuondoa zile zilizokufa, hivyo kupunguza ukavu na kutunza ngozi na kuifanya kungara na kuvutia.
7. Shea Butter
8. Karanga
Vyakula jamii ya karanga vina vitamin E ambayo ni muhimu katika kuzuia kuzeeka kwa ngozi hasa kutokana na kupigwa sana na jua. Vitamin E pia husaidia ngozi kuhifadhi unyevunyevu na hivyo kuifanya ngozi kuwa inang’aa na nyororo.
9. Maziwa ya Mbuzi
Maziwa ya mbuzi yana Vitamin A, E na Lactic acid. Lactic acid husaidia kuondoa seli zilizokufa kwenye ngozi na kuacha ngozi ikiwa na seli zilizo hai, hivyo kuifanya iwe na afya.
Maziwa ya mbuzi pia yana Caprylic Acid ambayo ni muhimu kwenye kupunguza kiwango cha asid kwenye ngozi – hii inasaidia kuzuia mazalia ya bakteria na vijidudu kwenye ngozi vilevile kusaidia ngozi kufyonza virutubishi kirahisi.
No comments:
Post a Comment